Mwanafunzi Akamatwa na Vocha za Vodacom za Tsh. Mil. 90
Kamanda wa polisi wa kanda maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
Sunday, September 27, 2009 5:14 PMMwanafunzi anayesoma chuo cha biashara cha CBE jijini Dar es Salaam amekamatwa pamoja na wenzake wawili akijaribu kuziuza vocha za wizi za kampuni ya simu ya Vodacom zenye thamani ya Tsh. Milioni 90.
Akiongea na waandishi wa habari, kamanda wa polisi wa kanda maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema kwamba mwanafunzi huyo wa CBE aliyejulikana kwa jina la Muhsini Amin mwenye umri wa miaka 21 alikamatwa pamoja na watuhumiwa wengine wawili Sadick Jediwa (21) mkazi wa Tandale na Rashidi Maulidi (28) mkazi wa Mwananyamala wakijaribu kuziuza vocha hizo.Kamanda Kova alisema kwamba watuhumiwa hao walikamatwa kwenye viwanja vya Leaders Club wakijaribu kuziuza vocha hizo za Ths. 10,000 na Tsh. 5,000 zenye thamani ya jumla Tsh. Milioni 90.Kova aliendelea kusema kuwa watuhumiwa hao walinaswa na polisi kufuatia mtego uliowekwa na polisi baada ya kupewa taarifa.Kova alisema kwamba polisi aliyejifanya mnunuzi wa vocha hizo alifanikiwa kuafikiana na watuhumiwa hao kuzinunua vocha hizo za Tsh. Milioni 90 kwa malipo ya nusu ya pesa hizo Tsh. Mil. 45.Watuhumiwa hao walikamatwa na kushikiliwa na polisi huku polisi ikiendelea na uchunguzi kugundua walizipata vipi vocha nyingi kiasi hicho.
Na Chondoma Shdabani, Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment